
KUPIGANA UWANJANI NI USHAMBA, MUDA WAKE UMEISHA
JUMA lililopita kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba na Ihefu FC kuna kipande cha video kilisambaa kikionyesha kundi la mashabiki wa Simba wakimshushia kichapo shabiki aliyefahamika kuwa ni wa Yanga kutokana na rangi ya mavazi yake. Vitendo hivi kuna nyakati vilishamiri na tulipaza sauti vikapotea lakini hivi sasa vinaonekana kurejea tena kwa…