Home Sports KI KAWAPOTEZA WENGINE NDANI YA YANGA

KI KAWAPOTEZA WENGINE NDANI YA YANGA

KWENYE msako wa kuwania tuzo ya mchezaji bora ndani ya kikosi cha Yanga Oktoba ni Stephane Aziz Ki ameshinda tuzo hiyo.

Kiungo huyo raia wa Burkina Faso alikuwa akiwania tuzo hiyo na nyota wengine wawili aliongia nao fainali.

Ni beki wa kazi Dickson Job na Max Nzengeli ambao walichaguliwa kuwania tuzo hiyo.

Aziz Ki atazawadiwa kiasi cha shilingi milioni 4 na tuzo kama ilivyobainishwa awali na mdhamini wa tuzo hiyo ambaye ni Kampuni ya NIC Insurance.

Kwenye ligi Aziz KI katupia mabao sita akiwa na pasi moja ya bao miongoni mwa timu alizozitungua ni Aza, FC alipowatungua hat trick Uwanja wa Mkapa kwenye Mzizima Dabi.

Previous articleKIVUMBI CHA LIGI KUU BARA KIPO HIVI
Next articleKUPIGANA UWANJANI NI USHAMBA, MUDA WAKE UMEISHA