
SINGIDA BIG STARS 0-2 YANGA
UBAO wa Uwanja wa Liti unasoma Singida Big Stars 0-2 Yanga ikiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara, mzunguko wa pili. Singida Big Stars imeshuhudia mabao yakifungwa kipindi cha kwanza cha mchezo huo ambao unafuatiliwa na mashabiki wengi duniani. Ni Aziz KI alipachika bao la kwanza kwa shuti kali ambalo lilimpoteza mlinda mlango Benedickt Haule…