KOCHA UNITED AAMBIWA AONDOKE TU HAMNA NAMNA

RIO Ferdinand, beki wa zamani wa Klabu ya Manchester United amesema kuwa kwa sasa ni muda mzuri kwa Kocha Mkuu, Ole Gunnar Solskjaer, kuondoka ndani ya kikosi hicho kwa heshima kabla ya kutimuliwa.

Beki huyo hapo awali alikuwa yupo upande wa kocha huyo kwa kuwa alikuwa akimtetea na alikuwa anaamini kwamba anaweza kuja kufanya vizuri ila mambo yamekuwa tofauti na vile ambavyo alikuwa anafikiria

Rio amecheza kwenye kikosi cha United na amekuwa ni mtu wa karibu na Ole ila anaamini kwamba kwa sasa muda wa kocha huyo kuwa ndani ya timu hiyo umeisha.

“Nafikiri kwa sasa ni muda wake wa kuondoka, ameshafanya kazi kubwa sana kwenye timu hii nadhani akiondoka kwa muda huu itakuwa ameondoka kwa heshima kubwa,”

Ole alijiunga na United Desemba 2018 na hajatwaa kombe lolote mpaka sasa yupo kwenye presha kubwa ya kibarua chake kuota nyasi na hivi karibuni amepoteza michezo minne kati ya sita ambayo aliongoza kikosi hicho kucheza.