>

AZAM FC KUSAJILI MASHINE TATU ZA KAZI

WAKATI vijana wa Azam FC wakiendelea na mazoezi kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu Bara msimu wa 2021/22, imeelezwa kuwa mabosi wa timu hiyo wapo kwenye mpango wa kusajili nyota watatu wa kazi kuongeza nguvu kwenye kikosi hicho.

Mpango kazi unatajwa kuchorwa kwa kuwafuata nyota kutoka Rwanda kwa lengo la kuboresha kikosi hicho ambacho kimeanza kwa kasi ya upole ndani ya Ligi Kuu Bara.

Kikiwa chini ya Kocha Mkuu, George Lwandamina eneo la ushambuliaji limeonakana kupoa kwa kuwa kwenye mechi tano ambazo ni dakika 450 safu ya ushambuliaji imefunga jumla ya mabao manne huku bao moja likifungwa na beki ambaye ni Daniel Amoah.

Habari zinaeleza kuwa bado muunganiko wa washambuliaji wapya unampa tabu Idd Seleman,’Nado’ ambaye alikuwa na ushkaji mkubwa na Prince Dube ambaye kwa sasa ni majeruhi.

Mmoja wa mabosi wa Azam FC ameweka wazi kuwa Azam FC inatafuta kiungo mmoja matata sana,beki wa kazi chafu pamoja na mshambuliaji wa kufunga mabao kila mechi.