ANTONIO RUDIGER ASANI MIAKA MINNE REAL MADRID

REAL Madrid imempa dili la miaka minne beki wa kazi akitokea Klabu ya Chelsea ambayo alikuwa akiitumikia.

Ni Antonio Rudiger amejiunga bure na Mabingwa wa Ligi ya Ulaya ambao waliinyoosha kwa bao 1-0 Liverpool.

Nyota huyo ni raia wa Ujerumani amemaliza mkataba wake ndani ya Stamford Bridge na hakuwa tayari kuweza kuongeza dili jipya zaidi ya kuhitaji changamoto mpya.

Tangu mwaka jana Real Madrid ilikuwa inasaka saini ya beki huyo na hatimaye imeweza kumpata kwa ajili ya msimu mpya wa 2022/23.

Anatarajiwa kutambulishwa rasmi Juni 20 katika Uwanja wa Santiago Bernabeu.

Madrid wamesema:”Real Madrid imefikia makubaliano ya kumsajili Antonio Rudiger na atatambulishwa rasmi jijini Madrid kupitia vyombo vya habari,”.