USIKU wa kuamkia leo Barcelona imeibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Athletic Club.
Mabao ya Pierre Aubameyang dk 37,Ousmane Dembele dk 73, Luuk de Jong dk 90 na Memphis Depay dk 90+3 yalitosha kuipa pointi tatu Barcelona.
Ilikuwa ni katika Uwanja wa Camp Nou mambo yote hayo yamefanyika.
Inakuwa na pointi 45 baada ya kucheza mechi 25 nafasi ya 4 na Athletic Club ipo nafasi ya 8 na pointi 37 baada ya kucheza mechi 26 ndani ya La Liga.