PRINCE DUBE NA NYOTA HAWA WATATU KUIKOSA YANGA

UKISUBIRIWA muda tu kwa sasa kwa matajiri wa Dar, Azam FC kumenyana na Yanga leo Uwanja wa Mkapa nyota wake wanne wanatarajiwa kuukosa mchezo wa leo kutokana na sababu mbalimbali.

Mchezo wa leo ni wa Ligi Kuu Bara ambapo kila timu inapambana kuweza kufikia malengo iliyojiwekea kwa msimu wa 2021/22.

Kwa mujibu wa Vivier Bahati, Kocha Msaidizi wa Azam FC amesema kuwa wanatambua mchezo huo utakuwa na ushindani ila wataingia kwa mtindo tofauti kwenye kusaka ushindi.

“Prince Dube amerudi lakini hatakuwa sehemu ya mchezo kwa sababu huwezi kumuandaa mchezaji kwa ajili ya mchezo mmoja, pia Sure Boy, (Salum Abubakar), Agrey Morris na Mudhathir Yahya hawa wataukosa mchezo kwa kuwa bado hawajajiunga katika mazoezi na suala lao lipo katika uongozi hilo siwezi kuzungumzia zaidi,” amesema.