Home Sports ISHU YA BANGALA KUIKOSA AZAM IPO HIVI, WENGINE HAWA HAPA

ISHU YA BANGALA KUIKOSA AZAM IPO HIVI, WENGINE HAWA HAPA

KUELEKEA katika mchezo wa Dabi ya Dar es Salaam leo Uwanja wa Mkapa kati ya Yanga dhidi ya Azam FC unaotarajiwa kuchezwa saa 1:00 usiku kuna baadhi ya mastaa wataukosa mchezo wa leo.

Miongoni mwa jina ambalo limekuwa likitajwa kwamba linaweza kukosekana ni pamoja na beki kitasa, Yanick Bangala jambo ambalo uongozi wa Yanga uliweza kulitolea ufafanuzi.

Kocha Msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze amesema kuwa wanatambua mchezo huo utakuwa mgumu lakini wanachohitaji ni pointi tatu muhimu huku suala la mchezaji wao Yanick Bangala kuwa na adhabu ya kadi watajiridhisha kwenye rekodi ili waoneka anazo ngapi.

Kuhusu wachezaji ambao watakosekana Kaze amesema:-“Yassin Mustapha bado hajawa fiti licha ya kwamba amepona, Mapinduzi Balama huyu alikuwa na maumivu ya muda mrefu,Dickson Ambundo huyu bado hajapona mkono ila anaendelea vizuri.

Alipoulizwa kuhusu uwepo wa Bangala kwenye kikosi hicho Kaze alisema:”Kuhusu Bangala ni mchezaji mzuri hivyo uwepo wake utategemea na ni kadi ngapi za njano ambazo anazo lakini katika hilo ni lazima tuweze kujihakikishia kwanza rekodi zinasemaje,” .

Mchezo wa leo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote mbili kusaka ushindi kwa kuwa msimu wa 2020/21 waligawana pointi tatutatu.

Walipokutana Uwanja wa Azam Complex, Yanga ilishinda bao moja na walipokutana Uwanja wa Mkapa, Azam FC ilishinda bao moja.

Previous articleKOCHA MJERUMANI AANDALIWA MIKOBA SIMBA, NDANI YA CHAMPIONI JUMAMOSI
Next articlePRINCE DUBE NA NYOTA HAWA WATATU KUIKOSA YANGA