Msichana wa Maisha Yangu ipo mezani tayari

BAADA ya kusubiri kwa muda ile simulizi nzuri ya maisha na masuala ya teknolojia kutoka kwa Best Seller Author, Lunyamadzo Mlyuka hatimaye kazi imefika mezani.

Ni yuleyule mtunzi wa Msichana wa Maisha Yangu na Moyo Wangu Unavuja Damu safari hii amekuja na kazi mpya inayoitwa Msichana wa Maisha Yangu.

Kwa ufupi kuhusu simulizi: Tatizo la ajira lilikuwa limeota sugu katika kichwa cha Steven ambaye awali kabla ya kufika Dar aliamini kila mtu mjini ana kazi nzuri na ana hela zakutosha. Alizunguka kila ofisi na bahasha yake ya khaki iliyokuwa na CV milango ilikuwa migumu mithili ya chuma cha pua.

Kuna siri nzito nzito kuhusu wadukuaji wa akaunti, mbinu wanazotumia, namna ya kujilinda na tatizo la udukuzi katika mitandao. Sio serikalini wala kampuni binafsi mfumo mkubwa ulikuwa unatumika hapo ndipo patashika na nguo kuchanika inatokea.

Kwa Steven kukosa anachokitafuta kulimfanya akumbwe na jambo jingine baya zaidi ambalo ni tatizo ya afya ya akili, mawazo yalimzidi uwezo hali hiyo ilipelekea apate ajali mbaya ya gari alipokuwa akivuka barabara ya Shekilango kituo cha Mapambano…

Ni nini hatma ya maisha yake na ujuzi alionao? Tatizo la ajira alilikabili namna gani? Majibu yote yapo katika kitabu cha Msichana wa Maisha Yangu.

Utajifunza Mbinu za kutumia kupata kazi, namna ya kubadili ujuzi kuwa fedha, afya ya akili, teknolojia ya AI,usaliti na hasara zake, matumizi sahihi ya muda na fedha…

Kutoka kwa Mtunzi wa Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu… 0756 028 371.