Simba SC yatambia taji la CRDB Federation Cup Jangwani

MARA baada ya kutwaa taji la CRDB Federation Cup Julai 4,2026 kwa ushindi wa bao 1-0 Azam FC, mabingwa Simba SC wametambia taji hilo kwa watani zao wa jadi.

Leo Simba SC wamefanya paredi la ubingwa huku wakipita mitaa mbalimbali walipoanza mapema saa 4:00 asubuhi wamepita mpaka makao makuu ya Yanga SC, Jangwani.

Baada ya kufika hapo mashabiki wa Simba SC walianza kucheza huku wengine wakienda Uwanja wa Kaunda walipofanyia burudani Yanga SC baada ya paredi Julai 4,2026.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC alinyanyua taji la CRDB Federation Cup na taji la Muungano ambalo walitwaa kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Yanga SC kwenye fainali.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, itakuwa mezani Julai 10,2026 jiandae kuipata.