Simba SC vs Singida Black Stars NBC Premier League ni mchezo unaofuata kwenye ratiba ya NBC Premier League, Juni 27, 2026 ukiwa ni mzunguko wa pili.
Mchezo huu unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Meja Jenerali Isahmuyo kwa wababe hawa kusaka pointi 3 muhimu ndani ya dakika 90.
Ni mchezo unaotoa taswira ya bingwa kupatikana mapema ama kusubiri mpaka mchezo wa mwisho raundi ya 30 kutokana na tofauti ya pointi 2 kati ya Yanga SC ambao ni vinara wenye pointi 69 na Simba SC nafasi ya pili wakiwa na pointi 67.
Steve Berkar, Kocha Mkuu wa Simba SC amesema wanatambua mchezo utakuwa mgumu lakini watapambana kufanya vizuri na kupata pointi 3 muhimu.
“Huu ni mchezo mgumu kwetu tutaingia kwa tahadhari kutafuta matokeo mazuri malengo ni kuona kwamba tunapata pointi 3 muhimu uwanjani,”.
Singida Black Stars ipo nafasi ya 4 baada ya mechi 28 imekusanya jumla ya pointi 50 kibindoni.
…
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.