Azam FC 3-2 Yanga SC

Azam FC 3-2 Yanga SC ni matokeo rasmi kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali CRDB Federation Cup katika mchezo uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza leo Juni 21, 2026.

Yanga SC walikuwa mabingwa watetezi wameangusha taji hilo ikiwa ni mara ya kwanza baada yakutetea kwa muda wa miaka mitano mfululizo.

Magoli ya Azam FC yamefungwa na Himid Mao aliyefungua ukurasa dakika ya 28, Lameck Lawi dakika ya 85 na Kitambala dakika ya 112.

Kwa upande wa Yanga SC magoli yalifungwa na Prince Dube dakika ya 67 na Bakari Nondo dakika ya 88 zikiwa zimesalia dakika 2 kugota dakika ya 90.

Hali hiyo ilipeleka mchezo kuongezwa dakika 30 kipindi cha ziada kusaka mshindi na kama asingepatikana kwenye muda huo mikwaju ya penati ingepigwa ila hatua hiyo haikufika mshindi alipatikana kwenye muda wa nyongeza.

Kwa matokeo hayo Azam FC atakutana na Simba SC kwenye mchezo wa fainali unaotarajiwa kuchezwa Julai 4, 2026.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.