Mbeya City 0-1 Simba SC, NBC Premier League, mchezo uliochezwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya Juni 17, 2026 kwa wababe hawa kupambania pointi 3.
Goli pekee ka ushindi limefungwa na winga Ellie Mpanzu dakika ya 43 kipindi cha kwanza limedumu mpaka mwisho wa mchezo.
Huu unakuwa ni mchezo wa 3 mfululizo Mpanzu anafunga kwenye NBC Premier League alianza mchezo vs Dodoma Jiji FC, Pamba Jiji FC na Mbeya City.
Matokeo haya yanaifanya Simba SC kupanda kutoka nafasi ya pili mpaka nafasi ya kwanza wakifikisha pointi 64 kibindoni.
Yanga SC inashuka mpaka nafasi ya pili ikiwa na pointi 63. Tofauti ya wababe hawa wawili ni pointi moja kwa sasa huku Yanga SC akiwa na faida ya mchezo mmoja mkononi.
Simba SC imecheza mechi 27 imesaliwa na mechi 3 huku Yanga SC ikiwa imecheza mechi 26 imesaliwa na mechi 4 kukamilisha msimu wa 2025/26 kutoka ligi namba 6 kwa ubora Afrika.
…
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.