Allan Okello kiungo mshambuliaji wa Yanga SC ni mtambo wa mabao ndani ya NBC Premier League 2025/26.
Nyota huyo raia wa Uganda ni ingizo jipya katika kikosi hicho akiwa ametambulishwa dirisha dogo ana uwezo wakufunga na kutengeneza pasi za magoli.
Ni magoli 11 na kutengeneza pasi 7 akihusika kwenye magoli 18 kati ya 60 ambayo yamefungwa na timu hiyo inayopambania kutetea taji la ligi.
Yanga SC imecheza jumla ya mechi 26, inaongoza kwenye ukali wakutupia magoli na imeruhusu magoli machache ambayo ni 9 sawa na Azam FC.
Okello, Mei 2026 alichaguliwa kuwa mchezaji bora kutokana na kiwango alichoonyesha, alifunga magoli 9 na pasi moja alitoa.
…
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.