MSAFARA wa kikosi cha Yanga SC umerejea salama Dar Juni 14, 2026 mara baada ya kumalizana na Mashujaa FC katika mchezo wa NBC Premier League uliochezwa Uwanja wa Lake Tanganyika, mwisho wa reli Kigoma.
Katika mchezo huo Juni 13, 2026 baada ya dakika 90 ubao ulisoma Mashujaa FC 0-2 Yanga SC, magoli yakifungwa na Mudathir Yahya na beki Bakari Nondo akihakikisha pointi zinarejea Dar.
Timu hiyo inaongoza ligi baada ya mechi 26 imekusanya jumla ya pointi 63 inafuatiwa na Simba SC yenye pointi 61 zote zimecheza mechi 26 zikisaliwa na mechi 4.
Tofauti ya wababe hawa wawili kwa sasa ni pointi 2 pekee na mwenye nafasi ya kutwaa ubingwa kwa asilimia kubwa ni Yanga SC kutokana na faida ya pointi 2 na idadi kubwa ya magoli ambayo amefunga.
Nahodha Bakari Nondo amesema kuwa malengo makubwa ni kuendelea kupata ushindi kwenye mechi ambazo zimebaki.
“Malengo nikuona kwamba tunapata matokeo kwenye mechi zetu ambazo zimebaki, mashabiki wawe nasi bado kazi inaendelea,”.
…
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.
Related News
Germany's defender #15 Nico Schlotterbeck celebrates after scoring his team's second goal during the 2026 World Cup Group E football match between Germany and Curacao at the Houston Stadium in Houston on June 14, 2026. (Photo by RONALDO SCHEMIDT / AFP)