SINGIDA Black Stars wamerejea mzigoni ikiwa ni maandalizi kuelekea mechi 5 ambazo zimesalia ndani ya NBC Premier League 2025/26.
Timu hiyo inapambana kumaliza katika nafasi nne za juu huku ikifuatiliwa kwa ushindani mkubwa na JKT Tanzania ambayo ipo nafasi ya 5.
Ukitazama msimamo unaonyesha Singida Black Stars nafasi ya 4 na pointi 41 inafuatiwa na JKT Tanzania nafasi ya 5 ikiwa na pointi 38.
Mchezo ujao kwenye NBC Premier League ni JKT Tanzania vs Singida Black Stars unatarajiwa kuchezwa Juni 13, 2026 Uwanja wa Meja Jeneral Isahmuhyo kwa wababe hawa kusaka pointi tatu muhimu.
Hussen Masanza, Ofisa Habari wa Singida Black Stars ameweka wazi kuwa wanafanya maandalizi kwa mechi zote ambazo zimebaki.
“Tunafanya maandalizi kwa mechi zote ambazo zimebaki ikiwemo mchezo wetu ujao dhidi ya JKT Tanzania, wachezaji wamerejea uwanja wa mazoezi tayari kwa kazi,”.
…
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.