Feisal anaongoza chati wafungaji Bongo

KIUNGO mshambuliaji wa Azam FC, Feisal Salum anaongoza chati ya wafungaji ndani ya NBC Premier League msimu wa 2025/26.

Kiungo huyo amefunga jumla ya magoli 11 akiwa anaongoza usukani katika chati ya wakali wa kucheka na nyavu ni mali ya Azam FC.

Kwenye eneo la ufungaji msimu huu ushindani umekuwa mkubwa huku kila timu ikiwa na nguvu katika eneo la ulinzi ndani ya uwanja.

Mpaka sasa hakuna mchezaji ambaye amefunga hat trick katika dakika 90 zaidi ya kuishia magoli mawili kwenye mechi na moja.

Namba mbili kwa utupiaji ni Prince Dube wa Yanga SC yeye amefunga magoli 9 kwenye ligi anafuatiwa na Ndumumwe Mossi wa Singida Black Stars, Fabrice Ngoy wa Namungo, Clatous Chama wa Simba SC na Seleman Mwalimu wa Simba SC hawa wote wamefung magoli 8.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.