Mashujaa FC vs Simba SC tambo zatawala

MASHUJAA FC vs Simba SC NBC Premier Leagu Mei 13, 2026 saa 10:15 jioni tambo zimetawala kwa wenyeji kubainisha wapo tayari kwa mchezo huo.

Kwenye msimamo Mashujaa FC ipo nafasi ya 9 ikiwa na pointi 26 inakutana na Simba SC iliyo nafasi ya pili na pointi 49 zote zimecheza mechi 22.

Steven Ndorobo, Ofisa Habari wa Mashujaa FC amesema kuwa wanatambua mchezo utakuwa mgumu lakini wamejipanga kupata pointi tatu mbele ya Simba SC.

Mchezo uliopita matokeo yalikuwa Simba SC 2-0 Mashujaa FC, Uwanja wa Meja Jeneral Isahmuyo kwa wababe hawa kukutana mzunguko wa kwanza ndani ya ligi namba 6 kwa ubora Afrika.

Ndorobo amesema: “Tunaendelea na maandalizi kuelekea mchezo wetu dhidi ya Simba SC, tupo tayari na kikubwa ni kuona kwamba tunapata pointi tatu muhimu,”.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC ameweka wazi kuwa mara baada ya ushindi dhidi ya Tanzania Prisons mpango ni kuendelea kushinda mechi zinazofuata.

“Tumepata ushindi dhidi ya Tanzania Prisons kituo kinachofuata ni Mei 14, 2026 dhidi ya Mashujaa FC tunahitaji kupata matokeo mazuri,”.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.