Simba SC 4-0 Tanzania Prisons ni matokeo ya mchezo wa NBC Premier League, Mei 10, 2026 uliokuwa na ushindani mkubwa.
Magoli yakifungwa na Morice Abraham dakika ya 27, Clatous Chama dakika ya 41, Seleman Mwalimu dakika ya 43 na Ismail Traore dakika ya 61.
Mwalimu alikosa penati dakika ya 11 baada ya Anthon Mligo kuchezwa faulo ndani ya 18 kwenye mchezo huo.
Man of The Match alichaguliwa kuwa Clatous Chama ambaye amesema kuwa ni furaha kuona wanapata matokeo mazuri kwenye mchezo mgumu.
Matokeo hayo yanaifanya Simba SC kufikisha jumla ya pointi 49 nafasi ya pili kwenye msimamo huku Tanzania Prisons ikisalia nafasi ya 15 na pointi 14 zote zimecheza mechi 22.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.