Clatous Chama amefunga magoli matatu Mei

Kiungo mshambuliaji wa Simba SC, Clatous Chama ametwaa tuzo ya Man of the Match mara baada ya mchezo. Mwamba wa Lusaka alifunga goli moja katika mchezo huo alikuwa kwenye ubora. Inakuwa ni tuzo yake ya tatu mfululizo kwenye mechi za Mei.

Alianza kukusanya tuzo Simba SC 2-2 Yanga SC, hapa alifunga goli moja na pasi moja ya goli. Simba SC 1-0 JKT Tanzania alifunga goli la ushindi. Simba SC 4-0 Tanzania Prisons alifunga goli moja na kutoa pasi moja ya goli kwa Traore kupitia pigo la kona.

Katika mechi 3 ambazo ni dakika 270, Chama amefunga magoli matatu na pasi mbili za magoli kati ya 7 ambayo yamefungwa. Mchezaji huyo amekuwa kwenye ubora mechi za mzunguko wa pili.

Ikumbukwe kwamba ni ingizo jipya katika dirisha dogo akitokea Singida Black Stars amekuwa ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Steve Berkar katika mechi za ushindani.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.