Yanga SC vs Coastal Union utachezwa mchezo mzuri leo Mei 9,2026 baada ya benchi la ufundi la wenyeji kubainisha hivyo.
Wananchi ni mabingwa watetezi wanatarajia kuvaana na Coastal Union kwenye mchezo wa NBC Premier League, leo saa 12:15, Uwanja wa KMC Complex.
Mchezo ulipita kwa Yanga SC ilipata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya KMC FC, mfungaji akiwa ni Allen Okello dakika ya 65.
Kocha Mkuu wa Yanga SC, Ahamid Moallin amesema kuwa wanatambua ugumu uliopo mbele ya wapinzani wao lakini watacheza mchezo mzuri na kumiliki mpira katika dakika 90.
“Kitu ninachoweza kuwaahidi mashabiki wa Yanga ni mchezo mzuri. Sisi kama Yanga tuna namna yetu ya mchezo. Msingi wa Yanga ni kumiliki mchezo. Tunawaheshimu Coastal Union lakini hatuwezi kuacha utamaduni wetu.
“Tunataka kumiliki dimba, sio kwa dakika chache bali kwa dakika zote 90. Kila mchezaji anapaswa kutoa alicho nacho kuhakikisha tunatawala mchezo na kupata matokeo mazuri,”.
Yanga SC inaongoza ligi ikiwa na pointi 51 mara baada ya mechi 21 inakutana na Coastal Union iliyo nafasi ya 13 na pointi 22.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.