Simba SC yatajwa kumpigia hesabu Chobwedo

INAELEZWA kuwa uongozi wa Simba SC upo kwenye hesabu za kuinasa saini ya kiungo wa TRA United Ramadhan Chobwedo.

Kiungo huyo amekuwa kwenye ubora katika mechi za hivi karibuni dhidi ya vigogo wa Kariakoo jambo ambalo linatajwa kuwavutia mabosi wa Simba SC.

Mbali na Simba SC imekuwa ikitajwa kuwa hata watani wa jadi wa timu hiyo, Yanga SC nao wanahitaji huduma ya kiungo huyo.

Tetesi zinaeleza kwamba ni Yanga SC walianza kumfuatilia mara baada ya mechi za mwanzo kwenye ligi kisha Simba SC wakafuata katika dili hilo.

Ni dau la milioni 150 linatajwa kuwekwa mezani ili kuipata saini ya kiungo huyo ambaye ana mwili jumba na upara kuwa sehemu ya utambulisho wake.

Taarifa rasmi bado hazijatoka kwa sasa kwa kuwa mchezaji ana mkataba na timu ya TRA United hivyo kwa timu ambayo inahitaji huduma yake lazima ikavunje mkataba na mabosi wake wa sasa.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.