PSG na Bayern Munich: Ni Kivumbi Ligi ya Mabingwa Leo Usiku Kwenye Uwanja wa Parc des Princes

Leo hii kuna mtanange wa kukata na shoka kati ya wenyeji PSG dhidi ya Bayern Munich kwenye Ligi ya Mabingwa. Je nani kutanguliza mguu kwenye Fainali msimu huu?

Ni usiku wa pambano kali leo kati ya PSG vs Bayern Munich kwenye uwanja wa Parc des Princes mechi ya Nusu Fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya huku wenyeji wakitaka kutetea taji lao.

PSG chini ya kocha mkuu Luis Enrique wanaingia uwanjani wakiwa na falsafa ya soka la kisasa linalojengwa juu ya umiliki wa mpira na ubunifu. Paris imekuwa timu inayopenda kudhibiti mchezo kuanzia nyuma, ikitengeneza mashambulizi taratibu lakini yenye madhara makubwa.

Kiungo chao kinachoongozwa na Vitinha ni injini ya timu, huku kasi ya Ousmane Dembele na ubunifu wa Khvicha Kvaratskhelia vikiwa silaha kuu za kuvunja ulinzi wa wapinzani. Pembeni, Achraf Hakimi huongeza kasi na tishio la mara kwa mara ndio maana kwenye safu ya ushambuliaji huwezi kuacha kuitaja timu hii wakiwa na Kombe 1 la UEFA hadi sasa.

Ukiachana mechi hiyo ya UEFA, Meridianbet inakwambia tengeneza mkwanja kupitia michezo ya Kasino ya Mtandaoni kama vile, Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli na mingine kibao. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Kwa upande wa Bayern Munich wao wakiwa chini ya kocha mkuu Vincent Kompany wamekuwa timu tishio barani Ulaya hadi sasa kutokana na mwenendo wao kwenye michuano yote hadi hii ya ligi ya mabingwa hadi sasa.

Bayern Munich wanakuja kwenye mechi hii wakiwa na uzoefu mkubwa kabisa, lakini pia ni timu ambayo imejengwa kwenye misingi bora ya kushambulia, ni timu ambayo inaweza kubadili matokeo muda owowte kutokana na ubora wa wachezaji ambao wanao hasa mbele kule wanapoongozwa na Harry Kane ambaye ni kinara wa mabao hadi sasa.

Kompany imezidi kuimarisha timu hii kwani amefanikiwa pakubwa sana hadi sasa tayari wao ni mabingwa wa BUNDESLIGA, walifanikiwa kutangazwa mabingwa wakiwa bado wana mechi 4 mkononi hapo ndipo unajua jinsi timu hii ilivyo tishio hadi sasa.

PSG na Bayern ni timu ambazo licha ya kuwa na safu bora kabisa za ushambuliaji, lakini ni timu ambazo kwenye upande wa mabeki imekuwa ni changamoto kwani kuruhusu mabao kwao imekuwa ni rahisi sana hivyo inaweza ikawa ni mechi yenye magoli mengi sana au laah magolikipa waamue kufanya kazi ya ziada zaidi.

Mechi hii inatarajiwa kuwa ya kisasi kwa vijana wa Luis Enrique kwani mara ya mwisho walipoteza mbele ya mabingwa hawa wa BUNDESLIGA hivyo hii inaweza ikawa ni nafasi yao ya kulipa kisasi. Je ni Kompany au Enrique kuanza vyema mechi hii ya Nusu Fainali pale Parc des Princes?

Kwa ujumla kabisa mechi hii ina kila dalili ya kuwa ya wazi, yenye nafasi nyingi na mabao kutoka pande zote mbili. PSG wana uwezo mzuri wa kushambulia halikadhalika kwa Bayern lakini tofauti inaweza kuja kwenye ufanisi nani atatumia nafasi zake vizuri zaidi.