Matokeo ya Simba SC Muungano Cup 2026

Simba SC imekata tiketi ya kutinga hatua ya fainali Muungano Cup 2026 kwa ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Mlandege FC katika mchezo nusu fainali ya pili.

Ushindi huo unaipata tiketi kukutana na Yanga SC kwenye mchezo wa fainali unaotarajiwa kuchezwa Aprili 29, 2026 Uwanja wa New Amaan Complex.

Ni wazi kwamba mabingwa watetezi wa taji la Muungano ni Yanga SC inayonolewa na Kocha Mkuu, Pedro Goncalves.

Simba SC ilifungua ukurasa  kwa matokeo ya ushindi ya Simba SC 1-0 Mafunzo SC hatua ya robo fainali.

Mchezaji wa kwanza kufunga goli ndani ya kikosi cha Simba SC Muungano Cup 2026 ni Seleman Mwalimu alifunga kwenye mchezo dhidi ya Mafunzo goli pekee la ushindi lililodumu mpaka mwisho wa mchezo.

Katika hatua ya nusu fainali alifunga goli la ufunguzi hivyo ni kinara wa ufungaji magoli ndani ya kikosi cha Simba SC akiwa na magoli mawili.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.