Singida Black Stars yaondolewa Muungano Cup

KLABU ya Singida Black Stars imeondolewa Muungano Cup 2026 kwa kufungashiwa virago na Mlandege FC leo Aprili 23, 2026 katika mchezo wa hatua ya robo fainali.

Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa New Amaan Complex umesoma Mlandege 2-1 Singida Black Stars magoli matatu yakifungwa.

Mlandege wamepindua meza kwa kuwa walianza kufungwa katika dakika ya 9 na Daud Mishamo katika kipindi cha kwanza goli ambalo lilidumu mpaka dakika ya 28.

Ni Musa Hassan maarufu kama Samatta alifungua ukurasa wa magoli kwa Mlandege dakika ya 28 na lile la pili lilifungwa na Mbappe dakika ya 45.

Samatta amechaguliwa kuwa mchezaji bora akizawadiwa milioni moja na wadhamini Chuo cha Afya cha Zanzibar School of Health.

Mabingwa watetezi wa Muungano Cup 2026 ni Yanga SC ambao watakutana hatua ya nusu fainali na Azam FC.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.