Ndoto za Chelsea za Ligi ya Mabingwa zatikiswa baada ya kupoteza kwa United

Bruno Fernandes aendelea kuwa shujaa wa Manchester United baada ya kutoa pasi ya bao (assist) lililoipa timu yake ushindi wa 1–0 dhidi ya Chelsea katika mchezo wa Ligi Kuu England uliochezwa Stamford Bridge usiku wa kuamkia leo Aprili 19, 2026.

Bao pekee la mchezo lilifungwa na Matheus Cunha kufuatia krosi nzuri kutoka kwa Fernandes. Hii ilikuwa assist yake ya 18 msimu huu, akikaribia kuvunja rekodi ya pasi za mabao (20) inayoshikiliwa na Kevin De Bruyne pamoja na Thierry Henry.

Licha ya kuwa na majeraha kwa mabeki wake kadhaa, United walionyesha nidhamu kubwa na kupata ushindi muhimu unaowaweka karibu kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya. Nahodha Fernandes ameendelea kuwa mhimili mkuu wa mafanikio yao.

Kwa upande wa Chelsea hali si nzuri:

Enzo Fernandez amerudi kikosini lakini amepokonywa unahodha msaidizi
Nafasi yake imechukuliwa na Moises Caicedo
Timu haijafunga bao kwa zaidi ya michezo minne ya ligi

Mashabiki wameanza kuonyesha hasira yao kutokana na matokeo mabaya, huku wakihofia kukosa nafasi ya kushiriki michuano ya Ulaya msimu ujao.