Azam FC 3-0 JKT Tanzania matokeo rasmi mchezo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex pointi tatu zikibaki kwa marajiri wa Dar.
Magoli ya Azam FC yamefungwa na Japhte Kitambala dakika ya 48 na Idd Seleman alifunga magoli mawili dakika ya 58 na 60 na alichaguliwa kuwa mchezaji bora.
Azam FC ipo nafasi ya 3 kwenye msimamo wa NBC Premier League ikiwa na pointi 37 baada ya mechi 19.JKT Tanzania nafasi ya 5 ikiwa na pointi 29.
Matajiri wa Dar ni Unbeaten katika mechi 19 ndani ya NBC Premier League msimu wa 2025/26 ambao una ushindani mkubwa.
Timu nyingine ambayo haijapoteza ndani ya ligi ni Yanga SC ambao ni vinara kwenye msimamo wakiwa na pointi 47 katika msimamo.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.