Neo Maema amepewa tuzo na kuonyeshwa kadi

NEO Maema amesema kuwa tuzo ambayo amepata katika mchezo wa NBC Premier League vs Coastal Union ni maalumu kwa mashabiki kutokana na uwepo wao kila mahali.

Aprili 2,2026 ubao wa Uwanja wa Meja Jeneral Isamuhyo ulisoma Simba SC 2-0 Coastal Union baada ya dakika 90 kukamilika.

Magoli yalifungwa na Seleman Mwalimu dakika ya 25 kwa pasi ya Clatous Chama na Ismail Traore dakika ya 45+2 kwa pasi ya Neo Maema.

Ni jumla ya kadi 3 za njano zilionyeshwa katika mchezo huo ambapo Coastal Union wachezaji wawili walionyeshwa G. Gwalala dakika ya 57 na L. Gradi dakika ya 55 kwa Simba SC akiwa Maema peke yake.

Maema alichaguliwa kuwa mchezaji bora na alionyeshwa kadi moja ya njano katika mchezo huo dakika ya 90.

Ni pointi 34 Simba SC inafikisha ikiwa nafasi ya pili baada ya mechi 15. Coastal Union nafasi ya 13 pointi 15 baada ya mechi 17.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.