Dodoma Jiji FC vs Fountain Gate ni leo Uwanja wa Airtel saa 8:00 mchana mchezo huo unatarajiwa kupigwa kwa wababe hawa wawili kusaka pointi tatu muhimu ndani ya dakika 90.
Uongozi wa Fountain Gate umebainisha kwamba umefanya maandalizi mazuri kwa ajili ya kuhakikisha wanapata pointi tatu dhidi ya Dodoma Jiji FC.
Huu ni mchezo wa ligi unaotarajiwa kuchezwa leo Aprili 3, 2026 ikiwa ni mzunguko wa 18 katika ligi namba 6 kwa ubora Afrika.
Issa Mbuzi, Ofisa Habari wa Fountain Gate iliyo nafasi ya 12 na pointi 16 amesema wanatambua wanakabiliana na Dodoma Jiji FC iliyo nafasi ya 9 na pointi 21 kwa hesabu ndefu.
“Tumetumia muda wa mapumziko kwa ajili ya maandalizi ya mechi zetu na tunaanza na Dodoma Jiji FC ugenini, Uwanja wa Airtel, tupo tayari na tunahitaji pointi tatu muhimu.
“Wakati wa mapumziko tulifanya mazoezi na tulicheza mechi za kirafiki na tulipata matokeo hivyo tunajiamini kuelekea mchezo wetu tukiwa ugenini,”.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.
Soccer Football - International Friendly - Spain v Brazil - Santiago Bernabeu, Madrid, Spain - March 26, 2024 Spain's Rodri scores their third goal from the penalty spot REUTERS/Violeta Santos Moura