Espérance Sportive de Tunis vs Simba SC CAF

Espérance Sportive de Tunis vs Simba SC CAF mchezo ujao kwenye ratiba kwa Simba SC inayofundishwa na Kocha Mkuu, Steve Barker.

Huu utakuwa ni mchezo wa kwanza kwa mrithi wa mikoba ya Dimitar Pantev kwenye anga la kimataifa msimu wa 2025/26.

Mchezo wa kwanza ilikuwa kwenye Ligi Kuu Bara ya NBC ambayo ni namba 6 kwa ubora Afrika ilikuwa dhidi ya Mtibwa Sugar walipogawana pointi mojamoja kwa ubao kusoma Simba SC 1-1 Mtibwa Sugar.

Kuelekea kwenye mchezo wa kesho kocha amebainisha kuwa wanatambua mchezo utakuwa mgumu lakini watapambana kupata matokeo mazuri.

“Tunatambua kwamba utakuwa mchezo mgumu lakini tupo tayari kwa mchezo na malengo ni kuona kwamba tunapata matokeo mazuri,”.

Miongoni mwa wachezaji wanaotarajiwa kuanza kikosi cha kwanza ni Clatous Chama ambaye amerejea kwa mara nyingine katika kikosi akitokea Singida Black Stars.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.