Meridianbet Yashirikiana na Jamii, Wasaidia Wajawazito na Waliojifungua

Katika kipindi ambacho afya ya mama na mtoto imeendelea kuwa ajenda muhimu ya kijamii, Meridianbet imejitokeza kuchukua nafasi yake kama mdau anayetoa mchango wa moja kwa moja. Kupitia mpango wake wa kijamii unaoendelea, kampuni hiyo imekuwa ikiwafikia akina mama wajawazito na waliojifungua, ikilenga kuwapa unafuu katika kipindi chenye uhitaji.

Msaada uliotolewa ulijikita katika vitu vinavyotumika kila siku na ambavyo vina athari kubwa kwa afya ya mama na mtoto. Vifaa hivyo vilihusisha nepi, nguo za watoto wachanga, wipes, sabuni pamoja na taulo za kike, vikilenga kuboresha afya, usafi na ustawi wa mama baada ya kujifungua.

Hatua hii ni sehemu ya utekelezaji wa sera ya Uwajibikaji wa Kampuni kwa Jamii (CSR) ya Meridianbet, inayotambua umuhimu wa sekta binafsi kushirikiana na jamii katika kukabiliana na changamoto za kijamii. Kwa mtazamo wa kampuni, kusaidia afya ya mama ni kuchangia moja kwa moja katika kizazi chenye afya na mustakabali imara.

 

Meridianbet haikuachi nyuma, kuna michezo mbalimbali ya kasino mtandaoni pamoja na mechi za kimataifa za kubashiri zenye odds bomba zinazokuongezea nafasi ya kuongeza kipato chako kila siku. Kujiunga ni rahisi! Tembelea meridianbet.co.tz au piga *149*10#.

Afisa Mawasiliano wa Meridianbet, Nancy Ingram, alisema kampuni inaamini kuwa mchango wa kweli huonekana pale unapogusa mahitaji ya msingi ya watu. Alieleza kuwa msaada huo umetolewa kwa nia ya kuwapa akina mama nguvu na matumaini wanapoanza safari ya malezi, hasa katika mazingira ya gharama za maisha zinazoendelea kupanda.

Kwa upande wao, wanufaika walieleza kuridhishwa na msaada huo, wakisema umefika wakati muafaka na utarahisisha maisha yao ya kila siku. Kupitia hatua hii, Meridianbet inaendelea kujijengea taswira ya kampuni inayochanganya huduma zake za michezo ya kubashiri na dhamira ya kweli ya kuinua ustawi wa jamii.