WAKIWA ugenini katika mchezo wa Premier League wiki ya 17 ubao wa Uwanja wa Tottenham Hotspurs umesoma Tottenham 1-2 Liverpool.
Magoli ya Hugo Ekitike dakika ya 66 na Isak dakika ya 56 yalikuwa na ya ushindi kwa Liverpool. Richarlison alipachika goli pekee kwa Tottenham dakika ya 83.
Mchezo huo Tottenham walionyeshwa kadi nyekundu wachezaji wawili Xavi Simon dakika ya 33 na Romero dakika ya 90+3.
Kadi za njano zilimwaga kwa wachezaji wa timu zote mbili ambapo ni Cristian Romero alionyeshwa kadi ya njano ya kwanza dakika ya 65 na ile ya pili dakika ya 90+3 ikaleta kadi nyekundu. Micky Van den Ven dakkka ya 85 alionyeshwa kadi ya njano , Rodrigo Bentancur dakika ya 90+5 kwa Tottenham.
Ibrahim Konate alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 77, Dominik Szoboszlai dakika ya 82 na Alexis Mac Allister dakika ya 90+7 kwa upande wa Liverpool walionyeshwa kadi za njano.
Mabadiliko
Ni Conor Bradley dakika ya 46 alimpisha Alexander Isak ambaye alikuwa super sub kwa kufunga goli la uongozi dakika ya 56. Alexander Isak alitoka dakika ya 60 akimpisha Jeremie Frimpong dakika ya 90.
Andy Robertson aliingia akichukua nafasi ya Hugo Ekitike dakika ya 90+9 na Treymaurice Nyoni aliingia dakika ya 90+10 akichukua nafasi ya Florian Wirtz ilikuwa ni kwa upande wa Liverpool.
Brenna Johnson dakika ya 58 aliingia akichukua nafasi ya Mohammed Kudus, Joao Palhinha aliingia dakika ya 71 akichukua nafasi ya Archie Gray, Wilson Odobert aliingia dakika ya 71 akichukua nafasi ya Lucas Gray na Richarlison aliingia dakika ya 80 akichukua nafasi ya Randal Kolo Muani.