POLISI TANZANIA 0-0 YANGA

VINARA wa Ligi Kuu Bara, Yanga leo wana kazi ya kusaka ushindi mbele ya Polisi Tanzania ambao nao pia wanahitaji ushindi.

Dakika 45 za kipindi cha awali zimekamilika na ubao wa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid unasoma Polisi Tanzania 0-0 Yanga.

Ni mchezaji mmoja anayeitwa Khalid Aucho ameonyeshwa kadi ya njano dakika ya 45 baada ya kumchezea faulo nyota wa Polisi Tanzania.

Metacha Mnata lango lake ndani ya dakika 45 za awali lipo salama kwa kuwa ameweza kutimiza majukumu yake ya kuzuia mpira kuingia wavuni.

Aboutwalib Mshery pia kwa upande wa Yanga lango lipo salama.