BEKI WA KAZI KIMENYA KUIKOSA AZAM FC

TANZANIA Prisons ikiwa imecheza jumla ya mechi 12 ndani ya Ligi Kuu Bara na kukusanya pointi 11 leo ina kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Azam FC.

Azam FC ipo nafasi ya 5 imecheza mechi 12 na kibindoni ina pointi 18.

Beki wa kazi chafu mwenye uwezo wa kupanda na kushuka, Salum Kimenya ataukosa mchezo wa leo Uwanja wa Nelson Mandela.

Sababu kubwa ni kusumbuliwa na nyama za paja hivyo bado hajawa fiti kwa sasa.

Katika mechi hizo 12 ambazo Prisons imecheza ni mechi 7 alianza kikosi cha kwanza msimu huu wa 2021/22.

Kimenya amesema kuwa kwa sasa anaendelea vizuri jambo ambalo anamshukuru Mungu.

Kila la kheri Kimenya