GHANA WAONDOLEWA AFCON

TIMU ya Taifa ya Ghana imeondolewa rasmi kwenye mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON 2021 na timu ya taifa ya Comoros katika mchezo wa mwisho wa Kundi C kwa kipigo cha mabao 3-2 katika mchezo uliopigwa Jumanne Januari 18.

Ghana ni washindi wa Kombe la Afcon mara nne wametolewa na timu ambayo ni mara yao ya kwanza kushiriki michuano hiyo mikubwa ngazi ya mataifa Afrika.

El Fardou Ben Nabouhane aliipa uongozi Comoros mapema ikafuatiwa na kadi nyekundu ya moja kwa moja iliyotolewa kwa mchezaji mashuhuri Andre Ayew.

Ahmed Mogni aliongeza bao la pili kwa wageni wa michuano Comoros kabla ya Ghana Black stars kupambana na kurudisha bao hizo na matokeo kuwa 2-2.

Hata hivyo, wakati dakika zikielekea jioni Ahmed Mogni alifunga goli la tatu kwa Comoros timu ya Visiwani ambayo inashika nafasi ya 132 kwenye viwango vya Fifa bao ambalo limefanya rekodi ya tangia mwaka 2006 kuvunjwa rasmi.

Ghana ilianza kwa matokeo ya kusuasua kwenye mashindano haya ambapo walianza na kipigo cha kufungwa bao 1-0 na Morocco kabla ya kutoa sare ya bao 1-1 na Gabon.

Nyota Andre Ayew aliweza kuonyeshwa kadi nyekundu dakika ya 25 na kufanya timu hiyo kuweza kukamilisha dakika 90 ikiwa na pungufu kwa timu hiyo iliyokuwa kundi C.