Kikosi cha Yanga SC dhidi ya Waangola Wiliete SC

YANGA SC Septemba 19 2025 itakuwa na kibarua mchezo dhidi ya Wiliete SC ya Angola ikiwa ni mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya awali.

Kwenye mchezo wa leo, Kocha Mkuu, Romain Folz ameanza na nahodha Bakari huku kiungo aliyefanya kazi kubwa mchezo uliopita dhidi ya Simba SC, Aziz Andambwile naye akianza moja kwa moja.

Aziz amekuwa ni chaguo la kwanza la kocha Romain kutokana na kuanza naye kwenye mechi muhimu za hivi karibuni.

Djigui Diarra, Israel Mwenda, Ladack Boka, Bakari Mwamnyeto, Ibrahim Bacca, Aziz Andambilwe, Clement Mzize, Duke Abuya, Mohamed Doumbia na Pacome Zouzoua wataanza kikosi cha kwanza.

Wachezaji wa akiba ni: Aboutwalib Mshery, Kibwana Shomari, Zimbwe Jr, Assinki, Balla Conte, Mudathir Yahya, Celestine Ecua, Edmund John na Maxi Nzengeli.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.