Msanii nyota wa muziki wa Bongo Fleva, Harmonize, ameendelea kuonyesha ubunifu na ubora wake katika tasnia ya muziki baada ya kuachia rasmi wimbo wake mpya uitwao “Best Couple”, akimshirikisha staa wa muziki kutoka Nigeria, Rudeboy (kutoka kundi la zamani la P-Square).
Wimbo huo umetoka rasmi usiku wa kuamkia leo Juni 27, 2025 na tayari umeanza kushika kasi mitandaoni, ukiwa na mdundo wa kimataifa unaochanganya ladha ya Afrobeats na Bongo Fleva. “Best Couple” ni wimbo wa kimapenzi unaosifia wapenzi wanaoelewana, kuheshimiana na kushikamana licha ya changamoto za maisha.
Harmonize kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii ameandika:
“Naamini huu ni wimbo utakaoeleweka kila kona ya Afrika… Asante Rudeboy kwa kolabo ya heshima. Let’s make history!”