HEINEKEN SILVER YAZINDULIWA KWA MBWEMBWE JIJINI DAR

Usiku wa kuamkia Juni 22, 2025, jiji la Dar es Salaam liligeuka kuwa kitovu cha burudani baada ya kufanyika kwa uzinduzi wa Heineken Silver kinywaji kipya kilichokuja na ladha laini lakini kisicho na mpinzani.

Uzinduzi huo umefanyika Mlimani City na uliandaliwa kwa ubunifu wa hali ya juu, na kuonyesha kiwango kipya cha hafla zenye hadhi ya kimataifa.

Zaidi ya wageni 400 walialikwa kushiriki katika tukio hilo la kipekee, akiwemo mastaa wakubwa wa Bongo, influencers maarufu, content creators wa kizazi kipya, pamoja na wapenda burudani kutoka kona zote za jiji.

Hakukuwa na sehemu ya VIP – kila mmoja alihudumiwa kama mgeni wa heshima, akipata huduma ya kifalme bila kujali jina au nafasi yake.

Wageni walitokelezea kwa mitindo ya kuvutia, wengi wakiwa wamevalia mavazi ya “Silver Futuristic”, yanayometameta kwa mwanga wa fedha na kuangaza usiku wa jiji. Mwonekano huu wa kisasa ulitengeneza ushindani wa aina yake, na mshindi wa vazi bora zaidi alizawadiwa Tsh milioni 2, akiondoka na sifa za usiku huo.

Kwa upande wa burudani, Chino Kidd alilishika jukwaa kwa umahiri wa hali ya juu – akiwasisimua wageni kwa perfomance kali na zenye nishati ya ajabu. Sauti, muziki na mwanga vilichanganyika kwa ustadi na kuumba usiku wa kukumbukwa.

Na kama hiyo haitoshi, vyakula na vinywaji vilitolewa bure kwa wageni wote – kuanzia vionjo vya kisasa vya kitafunwa hadi ladha halisi ya Heineken Silver iliyoambatana na kampeni yao mashuhuri ya #SmoothExperience.