AZAM FC YATAMBA KUIFUNGA SIMBA FAINALI

BAADA ya kufanikiwa kuibuka na ushindi wa penalti 9-8 dhidi ya Yanga katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi, uongozi wa Azam umetamba kuwa utaibuka na ushindi kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Simba na kuandika rekodi mpya kwenye michuano hiyo.


Hii inakuwa ni mara ya 
sita Azam kucheza fainali ya Kombe la Mapinduzi ambapo wamekuwa na rekodi nzuri katika michuano hii, wakifanikiwa kushinda fainali tano zilizopita.

Kwenye historia ya michuano hiyo Azam na Simba zimefanikiwa kukutana katika fainali tatu ambazo zote
zilimalizika kwa Azam 
kuibuka na ushindi mbele ya Simba, ambapo mara ya mwisho kufanya hivyo ilikuwa mwaka 2019.

Akizungumza na Championi Jumatano, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Azam, Zakaria
Thabith ‘Zaka Zakazi’ 
alisema: “Kwa pamoja, uongozi na benchi la ufundi tumefurahishwa na matokeo ya mchezo
wetu wa nusu fainali 
dhidi ya Yanga, kwetu hii inakuwa fainali ya sita ya michuano ya Mapinduzi ambapo tayari
tumeshacheza fainali tano 
za michuano hii.


“Kaimu kocha mkuu 
kwa sasa amewekeza nguvu katika kukiandaa kikosi dhidi ya mchezo wa fainali, tunaamini
utakuwa mchezo mgumu 
lakini nikuhakikishie kuwa tutawafunga na kuandika rekodi ya kuchukua taji hili kwa
mara ya sita,”.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Amaan saa 2:15 usiku.