IKIWA NA MOHAMED SALAH, MISRI YAPIGWA AFCON

NIGERIA wameipoteza Misri katika mchezo wa Kombe la Mataifa ya Afrika,’Afcon,’ ambapo baada ya dakika 90 ubao wa Roumde Adjia ulisoma Nigeria 1-0 Misri.

Licha ya uwepo wa staa anayekipiga ndani ya Liverpool,  Mohamed Salah,  Misri ilikwama kupata ushindi kwenye mchezo huo.

Bao la ushindi kwa Nigeria iliyo kundi D lilifungwa na Kelechi Iheanacho dakika ya 30 na lilidumu mpaka mwisho wa mchezo huo.

Nigeria walikuwa imara katika safu ya ushambuliaji kwa kuwa walipiga mashuti 15 na ni matano yalilenga lango huku Misri ikipiga mashuti manne na mawili yalilenga lango.

Nigeria sasa wanaongoza kundi wakiwa na pointi 3 huku Guinea Bissau ikiwa nafasi ya pili inafuatiwa na Sudan nafasi ya tatu hizi zina pointi moja na Misri ipo nafasi ya nne ikiwa na pointi 0.