ISHU YA KIBU KUTOFUNGA JEMBE AFUNGUKIA NAMNA HII

WAKATI kiungo mshambuliaji wa Simba akipukutisha mwaka bila kufunga ndani ya Ligi Kuu Bara, Legend kwenye masuala ya michezo Bongo na Kimataifa, Saleh Ally wengi wanamuita Jembe ameweka wazi kuwa hiyo sio kazi ya Kibu kufunga.

Ikumbukwe kwamba mara ya mwisho Kibu kufunga ilikuwa ni 5/11/2023 kwenye mchezo wa Kariakoo Dabi baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba 1-5 Yanga.

Kibu alifunga bao hilo dakika ya 9 akitumia pasi ya Said Ntibanzokiza kwenye mchezo huo uliokuwa na ushindni mkubwa zama za Miguel Gamondi.

Jembe amesema: “Kibu Dennis yeye kazi yake ni kuwatengenezea washambuliaji nafasi za kufunga na amekuwa akifanya hivyo kwenye mechi nyingi unaona namna ambavyo anapiga krosi na pasi zake kuwapa wengine.

“Kufunga sio kazi yake na ikitokea inakuwa ni bonus tu hiyo unaona namna alivyofunga dhidi ya Yanga na bao hilo likampa jina la mkandaji ila asingefunga angelaumiwa. Amerejea Simba na ameomba msamaha na amesamehewa ana kazi ya kuendelea kutimiza majukumu yake.”

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.