MABINGWA WATETEZI KOMBE LA MAPINDUZI WAWASILI ZANZIBAR

MABINGWA watetezi wa Kombe la Mapinduzi, Yanga leo Januari 4 wamewasili salama visiwani Zanzibar kwa ajili ya kuanza kazi ya kutetea taji hilo.

Yanga ilitwaa taji hilo mwaka 2021 kwa ushindi mbele ya Simba kwa mikwaju ya penalti baada ya dakika 90 kutoshana nguvu ya bila kufungana.

Kwenye mchezo huo kikosi cha Simba licha ya uwepo wa mshambuliaji wao namba moja Meddie Kagere kiliyeyusha dakika 90 bila kupiga shuti ambalo lililenga lango.

Yanga kazi yake ya kwanza inatarajiwa kuwa Januari 5 itakuwa dhidi ya Taifa Jang’ombe pia na Simba nayo itakuwa na kazi ya kusaka ushindi dhidi ya Selem View.