OFISA HABARI MPYA WA SIMBA AWASHUKURU MASHABIKI

OFISA Habari wa Simba SC, Ahmed Ally amewashukuru mashabiki wa klabu hiyo kwa mapokezi mazuri waliomuonyesha mara baada ya kutangazwa kuitumikia klabu hiyo jana, Jumatatu, Desemba 4, 2022.

Kupitia akaunti yake ya Instagram, Ahmed Ally ameandika; “Msemaji wa Mabingwa nimeamka salama.Kwa nafasi ambayo nimepewa nasema asante na nimefurahi kuwa hapa kwa kuwa ilikuwa ni ndoto yangu.

“Awali ya yote nisema asante Wana Simba kwa mapokezi makubwa niliyopata kutoka kwenu hii ni ishara kuwa mnanipenda, mnaniamini na mmenikubali nami niwahakikishie tuu sintawaangusha

“Mapokezi yenu yamenipa nguvu, faraja na matumaini ya kuwa niko sehemu sahihi na sehemu salama, sehemu ya watu wenye upendo wa hali ya juu hakika hii sio timu hii ni familia.

“Malengo yetu ni kuona kwamba tunaweza kuchukua Kombe la Mapinduzi kwa kuwa tumekuja kufanya kweli pia tunajezi mpya na nzuri sisi sio kauka nikuvae,” amesema.