Home Sports YANGA YAMALIZANA NA MKALI WA MABAO YA KIDEONI

YANGA YAMALIZANA NA MKALI WA MABAO YA KIDEONI

CRISPIN Ngushi, aliyekuwa mshambuliaji wa Mbeya Kwanza sasa rasmi ni mali ya Yanga.

Nyota huyo ndani ya Ligi Kuu Bara ametupia jumla ya mabao matatu na alikuwa ni kinara ndani ya Mbeya Kwanza.

Alikuwa ni mshambuliaji wa kwanza msimu wa 2021/22 kufunga bao la kideo ambalo ni Acrobatic ilikuwa mbele ya Mbeya City katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Sokoine.

Ni mkali wa mabao ya kideoni sasa ni rasmi ni kijani na njano akiwa amepewa dili la miaka miwili.

Anakuwa ni Mwananchi ambapo ametambulishwa usiku wa kuamkia leo baada ya kupewa dili hilo la kuwatumikia mabingwa watetezi wa Kombe la Mapinduzi.

Previous articleMABINGWA WATETEZI KOMBE LA MAPINDUZI WAWASILI ZANZIBAR
Next articleMUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMATANO