KIBU DENNIS AMEANZA BALAA, ATAFUTWE MWINGINE

KIBU Dennis kiungo mshambuliaji wa Simba amejihakikishia nafasi kikosi cha kwanza chini ya Kocha Mkuu, Fadlu Davids ambapo kwenye mechi mbili mfululizo alianza kikosi cha kwanza.

Katika Kariakoo Dabi, Kibu hakukomba dakika 90 lakini aliingia kwenye orodha ya nyota waliochezewa faulo zaidi ya tano ndani ya uwanja na mojawapo alisababisha kadi ya njano kwa Dickson Job.

Ilikuwa ni Oktoba 19 2024 baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba 0-1 Yanga bao la Maxi Nzengeli dakika ya 86.

Mchezo dhidi ya Tanzania Prisons alisepa na dakika 90 ambapo pigo lake la faulo dakika ya 5 lilimshinda mlinda mlango Mussa Mbisa kwenye harakati za kuokoa Che Malone akafunga bao lililoipa pointi tatu Simba.

Kwa namna ambavyo ameanza kurejea katika ubora, uwezo wa kufanya majaribio ndani ya uwanja Kibu Dennis sasa ni muda wa Simba kutafuta Kibu Dennis mwingine ambaye atavaa viatu vyake pindi asipokuwa fiti.

Kumbuka kwamba tayari amekuwa chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Fadlu Davids kwenye mechi za ushindani ndani ya msimu wa 2024/25.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.