KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Maxi Nzengeli anashikilia rekodi ya kuwa mfungaji wa bao la kwanza ndani ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2024/25 akiwa na uzi wa Yanga.
Bao hilo alifunga katika mchezo wa ligi dhidi ya Kagera Sugar uliochezwa Uwanja wa Kaitaba ilikuwa ni Agosti 29 2024 mabingwa hao watetezi walicheza mchezo wa kwanza wa ligi.
Chini ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi Maxi alianza kikosi cha kwanza na alipachika bao hilo akitumia pasi ya Pacome.
Gamondi alianza kikosi cha kwanza na Diarra mdaka mishale langoni, Boka, Bakari Mwamnyeto ambaye ni nahodha, Dickson Job nahodha msaidizi, Bacca beki wa kazikazi, Khalid Aucho, Maxi, Mudathir Yahya, Prince Dube, Aziz Ki na Pacome Zouzoua.
Bao la pili lilifungwa na Clement Mzize ambaye anaingia kwenye rekodi ya kuwa mchezaji mzawa wa kwanza kufunga ndani ya Yanga msimu wa 2024/25 akitokea benchi.
Septemba 6 2024 Maxi alikuwa miongoni wa wachezaji waliocheza mchezo wa kirafiki, Uwanja wa KMC Complex dhidi ya Cosmopolitans FC huku Yanga ikishinda kwa mabao 2-0.
Timu hiyo kwa sasa ipo kwenye maandalizi ya mchezo wa kimataifa dhidi ya Ethiopian Nigd Bank unaotarajiwa kuchezwa Septemba 14 2024 ambapo Yanga itakuwa ugenini.
Mchezo wa marudio unatarajiwa kuchezwa Uwanja qa Mkapa itakuwa ni Septemba 21 2024 ambapo mshindi wa jumla atasonga mbele katika hatua inayofuata.
Septemba 25 Yanga itakuwa na mchezo wa ligi dhidi ya Ken Gold itakuwa ugenini na mchezo wake wa kwanza ndani ya ligi kuwa nyumbani ni dhidi ya KMC itajuwa Septemba 29.
Ndani ha Septemba Yanga ina mechi nne za moto ambazo ni dakika 360 kusaka ushindi ambapo mbili ni anga la kimataifa na mbili ni kwenye ligi.