NABI:TUTAWAFURAHISHA MWAKA HUU ZAIDI

NASREDDINE Nabi,Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa kwa mwaka mpya wa 2022 watazidi kuwafurahisha zaidi mashabiki kwa kupata matokeo mazuri pamoja na kucheza soka safi.
Yanga imecheza mechi 11 bila kupoteza mchezo hata mmoja na kibindoni ina pointi 29 ikiwa ipo namba moja kwenye msimamo.
Ni ushindi wa mabao 4-0 walipata jana Desemba 31 kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Dodoma Jiji.
Nabi amesema kuwa anapenda kutuma ujumbe kwa mashabiki na Watanzania wote kiujumla juu ya mwaka mpya 2022 na malengo yao yapo palepale kuendelea kupata matokeo safi.
“Ninapenda kuwaambia mashabiki wote wa Yanga na Watanzania kiujumla heri ya mwaka mpya 2022 lakini kikubwa ni kwamba bado tutaendelea kuwafurahisha na kucheza soka safi ambalo litatupa matokeo mazuri.
“Watanzania ni wakarimu na ninapenda namna ambavyo wanapenda mpira kwa kuwa mimi sio mtu wa manenomaneno basi kazi inaendelea bila matatizo,” amesema Nabi.