UWANJA wa Mkapa, Januari Mosi,2022 mchezo wa Ligi Kuu Bara umekamilika kwa Simba kufungua mwaka kwa kusepa na pointi tatu mazima.
Baada ya dakika 90 ubao umesoma Simba 2-1 Azam FC.
Mabao ya Sadio Kanoute na Sakho kwa Simba huku bao la Azam FC likifungwa na Zulu.
Katika mchezo wa leo mpaka muda mapumziko timu zote mbili zilikwenda vyumba vya kubadilishia nguo wakiwa hawajafungana.
Rally Bwalya alikosa penalti baada ya kipa wa Azam FC kuweza kuipangua.