KICHAPO CHA LIVERPOOL CHAMUIBUA KLOPP

JURGEN Klopp, Kocha Mkuu wa Liverpool amesema kuwa hajapendezwa na matokeo ya timu hiyo kupoteza kwa kufungwa mbele ya Leicester City.

Usiku wa kuamkia leo Desemba 29 ubao wa Uwanja wa King Power ulisoma Leicester City 1-0 Liverpool.

Bao la Ademola Lookman dakika ya 59 lilitosha kuwapa pointi tatu mazima.

Licha ya Liverpool kupiga jumla ya mashuti 21 huku manne yakilenga lango haikufua dafu kwao kupata pointi wakati ni mashuti sita walipiga Leicester City na moja lililenga lango likajaa wavuni.

Klopp amesema:”Hatukutaka kuwa hivyo lakini imetokea ni mbaya kwetu tutazidi kupambana,”.

Liverpool ipo nafasi ya pili ba pointi 41 huku Leicester City ikiwa nafasi ya 9 na pointi 25.